Muungano wa Sayansi #GatesLetter Big Bet Challenge

Sisi katika Muungano wa sayansi ni azimio letu kwamba miaka kumi na tano kutoka sasa bioteknolojia za kilimo zinazokuzwa na wanasayansi wa sekta ya umma zitaleta maendeleo katika maisha ya watu duniani. Miaka kumi na tano kutoka sasa wakulima wote duniani watapanda mimea ambayo inahitaji dawa chache za wadudu wa mimea na viongezi vya kemikali. Nao mchele ndizi na mihogo iliyoimarishwa kibiolojia itaboresha lishe kwa mabilioni ya watu. Mbiringanya na kunde zenye BT zitapunguza matumizi ya dawa za wadudu wa mimea hivyo basi kunufaisha wakulima, watumizi wa mazao na mazingira. Mimea nayo itastawi katika hali ya hewa isiyotabirika kwa hivyo kuhimili joto ukame wadudu na magonjwa na pia kuweza kutumia kwa ufanisi zaidi rasilimali chache kama nitrojeni na maji. Sisi katika Muungano wa sayansi ni azimio letu kwamba katika miaka kumi na tano kutoka sasa watu kutoka kila sehemu watakuwa wameweza kutumia mbinu bunifu ambazo zitaboresha mazingira, usalama wa chakula na pia maisha duniani.
Narrated by: Angela Siele
Special thanks: Tom Mbega


Categories